Wakati mgunduzi wa mtandao wa Facebook bwana Mark Zuckerberg akiwa busy na mtandao wake wa Facebook, wadukuzi walikuwa busy kudukua akaunti zake za twitter na pinterest.

Wadukuzi hao kutoka Saudi Arabia inasemekana walitumia taarifa za kiusalama zilizovuja mtandaoni kutoka katika mtandao wa linkedin. Kikundi hicho kinachojiita OurMine Team kilidukua akaunti ya Zuckerberg mapema jumapili hii.